EID MUBARAK
Salamu zangu za Eid kwa waislam tuliomo humu Kwanza tunamshukuru Allah s.w kwa kutuwezesha kukamilisha ibada hii muhimu kwa wale tuliojaaliwa kukamilisha Na Allah awajaalie wale wote ambao kwa sababu mbalimbali hawakuikamilisha, InshaAllah Allah Awajaalie mwakani mwakani waikamilishe Usia wangu kwangu na kwenu sote tujitahidi kukamilisha Sitat shawal kwani mwenye kufanya hivyo atshesabiwa kuwa amefunga mwaka mzima MashaAllah Aidha leo si siku ya kufurahia hadi kumuaswi Allah tabaarak kwani mwenye kufanya hivyo atakua amemuaswi Allah mfano wa siku ya hesabu (Qiama) yaani mbele yake Allah s.w Kubwa zaidi tuyaenzi na tuyaishi yale maisha tuliyokuwa tukiishi ndani ya mwezi mtukufu wa Ramadhan kwani ndio maisha ambayo Allah s.w ameelekeza kuyaishi Ifahamike kuwa Ramadhani imeondoka lakini Allah s.w hajaondoka na yupo Tuwe wachaMungu na tufanye ibada ya *Swala tano* na ibada nyingine zilizofundishwa na fahamu kuwa kuacha swala kwa makusudi ni ukafiri ulio wazi kabisa *Tofauti ya muislam...