TETESI ZA USAJILI AUGUST 9


 Mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi, 34, amepangwa kufanyiwa vipimo vya matibabu hii leo Jumatatu kabla ya kukamilisha uhamisho wa bure kwenda Paris St-Germain. (L'Equipe - in French) 


Messi atazinduliwa kama mchezaji wa PSG kwenye hafla maalum katika Mnara wa Eiffel katika siku chache zijazo.(ESPN) 


Barcelona wanajaribu kuzuia jaribio lolote la PSG kumsaini Messi kwa kufungua malalamiko kwa Tume ya Ulaya ikisema kilabu hiyo ya Ufaransa itakiuka sheria za matumizi ya fedha ikiwa watafanikiwa kumsajili Muargentina huyo. (Marca, in Spanish) 


Tottenham ni miongoni mwa vilabu ambavyo vimejaribu kumsajili Messi baada ya Barca kusema hatosalia Nou Camp. (Express) 


Arsenal iko tayari kufanya kufanya usajili wa beki wa Atletico Madrid Kieran Trippier kwani Manchester United imeshindwa kukubaliana ada na mabingwa wa Uhispania kwa mchezaji huyo wa England mwenye umri wa miaka 30. (Sun) 


Kocha wa Roma, Jose Mourinho anataka sana kumsajili mshambuliaji wa Paris St-Germain wa Argentina mwenye umri wa miaka 28, Mauro Icardi, huku Edin Dzeko wa Bosnia, 35, akionekana kukaribia kuondoka mji mkuu wa Italia kwenda Inter Milan. (Gazzetta dello Sport - in Italian) 


Dzeko anakaribia kuhamia San Siro kama mbadala wa mshambuliaji wa Ubelgiji Romelu Lukaku, 28, ambaye yuko mbioni kurudi Chelsea. (sun)

Arsenal inashindana na Tottenham kuwania saini ya mshambuliaji wa Fiorentina wa Serbia Dusan Vlahovic, huku Spurs ikimtaka mchezaji huyo wa miaka 21 kama mbadala wa Harry Kane, ambaye anatafutwa na Manchester City. (Sky Sport Italia's Gianluca Di Marzio - in Italian) 


Manchester United wanajiandaa kutoa ombi la kupata huduma za mshambuliaji wa Ufaransa wa miaka 30 Antoine Griezmann. (Todofichajes - in Spanish)

Maoni

Chapisha Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

TAULO

EID MUBARAK