TETESI ZA USAJILI AUGUST 9
Mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi, 34, amepangwa kufanyiwa vipimo vya matibabu hii leo Jumatatu kabla ya kukamilisha uhamisho wa bure kwenda Paris St-Germain. (L'Equipe - in French) Messi atazinduliwa kama mchezaji wa PSG kwenye hafla maalum katika Mnara wa Eiffel katika siku chache zijazo.(ESPN) Barcelona wanajaribu kuzuia jaribio lolote la PSG kumsaini Messi kwa kufungua malalamiko kwa Tume ya Ulaya ikisema kilabu hiyo ya Ufaransa itakiuka sheria za matumizi ya fedha ikiwa watafanikiwa kumsajili Muargentina huyo. (Marca, in Spanish) Tottenham ni miongoni mwa vilabu ambavyo vimejaribu kumsajili Messi baada ya Barca kusema hatosalia Nou Camp. (Express) Arsenal iko tayari kufanya kufanya usajili wa beki wa Atletico Madrid Kieran Trippier kwani Manchester United imeshindwa kukubaliana ada na mabingwa wa Uhispania kwa mchezaji huyo wa England mwenye umri wa miaka 30. (Sun) Kocha wa Roma, Jose Mourinho anataka sana kumsajili mshambuliaji wa Paris St-...